ASKARI POLISI WANNE WATIWA MBARONI MWANZA


Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ahmed Msangi ametoa amri kukamatwa kwa askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha Polisi Nyamagana kutokana na asakri hao kumjeruhi kwa risasi mke wa Mwenyekiti mtaa.

Kamanda Msangi amesema polisi hao tayari wametiwa mbaroni kwa kumjeruhi kwa risasi mguuni Bi. Editha Ntobi ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Majengo Mapya uliopo katika Kata ya Mabatini jijini Mwanza.

Msangi amesema polisi hao wanatuhumiwa kufyatua hovyo risasi zaidi ya 10, kuharibu mali za raia lakini pia wanadaiwa kufanya matukio hayo kutokana na kulewa wakati wakiwa kwenye doria kinyume na utaratibu wa kazi yao.

Bi Editha Ntobi ambaye ni majeruhi wa kupigwa risasi amelazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza kutokana na kuvuja kwa damu nyingi kufutia tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527