Picha: MAONESHO YA BIASHARA YA FAHARI YA GEITA YAWA KIVUTUO KIKUBWA



Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa maonesho ya Biashara ya Fahari ya Geita ambayo kwa mwaka huu katika viwanja vya Kalangalala ikiwa ni awamu ya Pili tangu kuanza Mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na meneja mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw,Manase Ndoroma wakati akiwasili kwenye viwanja vya maonesho. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na kuteta jambo na Meneja wa NSSF Mkoani Geita Shabaan Mpendu , wakati akiwasili kwenye viwanja vya maonesho. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akisaini kitabu cha mahudhulio kulia ni mwenyekiti wa maandalizi ya maonesho ya fahari ya Geita Raphael Siyantemi ,kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Leornad Kiganga Bugomola. 
Mwenyekiti wa maandalizi ya maonesho ya fahari ya Geita Raphael Siyantemi,akitoa utambulisho kwa mgeni rasmi na kuwashukuru wafadhili ambao wamejitolea fm,Mgodi wa dhahabu wa Geita,NSSF,Clouds media Group WAJA na wengineo.
Meneja mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw,Manase Ndoroma ,akiwawakilisha wafadhili ambao wamehusika kufadhili maonesho hayo ya Biashara pamoja na kusisitiza wao kama Mgodi wataendelea kushirikiana na wadau wa maonesho hayo kwa kutoa ufadhili pamoja na kushiriki kwa kila mwaka. 
Mchezaji wa Ngoma za asili kutoka Wilayani Chato akitoa Burudani wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Biashara Mkoani Geita. 
Msanii wa vichekesho ambaye anajulikana kwa jina la Mfupi kwenda chini akituzwa wakati alipokuwa akitoa burudani kwenye maonesho. 
Kikundi cha Vichekesho cha Futuhi wakitoa Burudani . 
Brother K maarufu kwa jina la Tajiri wa Kigoma wa kikundi cha Futuhi akiendelea kufanya yake. 
Baadhi ya mabanda ambayo yapo kwenye maonesho. 
Mgeni rasmi,ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Meje Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akipatiwa maelezo na afisa wa Polisi Bi,Esnart Magoti wakati alipotembelea Banda la Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama Barabarani. 
Afisa Masoko na uhusiano wa NSSF Makao makuu,Bi Aisha Sango akitoa maelezo kwa Mgeni Rasmi namna ambavyo wamekuwa wakitoa huduma na kusajili baadhi ya watu ambao wanajiunga na mfuko wa Bima ya Nssf. 

Meneja wa NSSF Mkoani Geita Shabaan Mpendu ,akielezea juu ya mfuko wa NSSF ambavyo wameendelea kuboresha huduma za mfuko huo siku hadi 
Lango ka kuingilia kwenye maonesho ya Biashara ya Fahari ya Geita.
Picha Zote na Joel Maduka wa Maduka Online. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527