KAULI YA SPIKA WABUNGE LA TANZANIA BAADA YA KUPOKEA BARUA YA WABUNGE 8 KUFUKUZWA UANACHAMA CUF

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema amepokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ya kuwafukuza uanachama wabunge wanane wa chama hicho.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Jumanne, Julai 25, Spika amesema suala la kuwaondoa wanachama ni la utashi wa vyama vyenyewe na kila chama kina utaratibu wake.

“Hivyo bado naendelea kuitafakari barua hiyo na taarifa rasmi kuhusu maamuzi yangu kwa wabunge waliofukuzwa nitaitoa hapo baadaye,” amesema.

Wabunge waliofukuzwa uanachama na Lipumba ni Silvanus Mwijage, Saumu Heri Sakala, Salma Mwassa, Riziki Shahari Ngwali na Raisa Abdallah Mussa.

Wengine ni Miza Bakari Haji, Hadija Salum Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed, (MB).

Miongoni mwa makosa yaliyotajwa katika barua ya Lipumba ni pamoja na wabunge hao kukihujumu chama katika uchaguzi wa marudio wa madiwani wa tarehe 22 Januari, 2017 na kumkashifu na kumdhalilisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, (Lipumba).

Makosa mengine ni kumkashifu Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya, (MB) pamoja na wakurugenzi wa chama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527