TAMKO LA SHIRIKA LA SHINYANGA DERIVATIVE DEVELOPMENT ORGANIZATION (SDDO) KATIKA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU DUNIANI


Afisa Uhusiano wa Asasi isiyo ya kiserikali inayotambulika kama Shinyanga Derivative Development Organization (SDDO), Zaituni Mshana akizungumzia kuhusu kampeni ya uchangiaji damu inayotarajiwa kufanywa na asasi hiyo mkoani Shinyanga.

TAMKO LA SHIRIKA LA SHINYANGA DERIVATIVE DEVELOPMENT ORGANIZATION (SDDO) KATIKA SIKU YA UCHANGIAJI DAMU DUNIANI TAREHE 14/06/2017.

 Ndugu Wanashinyanga na Watanzania kwa ujumla tulioko mbele yenu ni wawakilishi wa Asasi isiyo ya kiserikali inayotambulika kama SHINYANGA DERIVATIVE DEVELOPMENT ORGANIZATION kwa kifupi (SDDO) iliyosajiliwa kisheria na kupewa usajili wa kufanya kazi zake ndani ya Tanzania bara.

 Ofisi zetu zinapatikana katika jengo la CCM mkoa wa Shinyanga,Chumba namba 210 katika manispaa ya Shinyanga ndani ya Mkoa wa Shinyanga,Asasi ya SDDO inafanya kazi za kijamii ikiwa na malengo makuu ya kupunguza kama siyo kuondoa kabisa umaskini na njaa ndani ya jamii ya watanzania.

 Ndugu Watanzania kwa kutambua umuhimu wa siku ya Uchangiaji damu duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Tarehe 14/06,SDDO tunawaomba na kuwahamasisha kujitokeza kuchangia damu kila tupatapo nafasi. 

SDDO tumekusudia kuendesha kampeni ya uchangiaji damu ndani ya mkoa wa Shinyanga katika wilaya za Shinyanga ambazo ni Kahama,Shinyanga na Kishapu ili kuweza kupunguza tatizo la upungufu wa damu katika benki ya damu,hivo tunawaomba wadau kuweza kushirikiana nasi katika kuendesha zoezi hilo na kutimiza kauli mbiu ya “CHANGIA DAMU,CHANGIA SASA,CHANGIA MARA KWA MARA”, na kuunga mkono jitihada za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto chini ya Waziri Mheshimiwa Ummy Mwalimu.

Kumbuka damu zitakazokusanywa nchini zitasaidia kuokoa vifo vya kina mama,watoto chini ya miaka mitano,waathirika wa ajali na magonjwa mengine kama saratani.

 Changia damu kwa hiari,changia damu bila malipo,wananchi wa mkoa wa Shinyanga tujitokeze kwa wingi pindi kampeni zitakapoanza.

 SDDO-WE DERIVE POTENTIALS.
 
Afisa Uhusiano wa SDDO, Zaitun Mshana akizungumza na waandishi wa habari leo June 14,2017
Afisa Uhusiano wa SDDO, Zaitun Mshana akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa damu salama mkoa wa Shinyanga,Elizabeth Shilla katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambaye alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa damu salama kwani hivi sasa wanapata chupa zisizozidi 250 kwa mwezi ambapo mahitaji ni zaidi ya chupa 400 kwa mwezi hivyo kutumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu
Mtaalamu wa damu salama mkoa wa Shinyanga,Elizabeth Shilla akiendelea kutoa maelezo
Maafisa kutoka SDDO wakiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments