RIPOTI : KAMPUNI YA ACACIA HAINA KIBALI NA INAFANYA KAZI KINYUME CHA SHERIA


Taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais John Pombe Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.

Prof. Osoro amesema Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.

Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.

Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini kwenye makontena yote 44,277 tangu mwaka 1998 ni Tsh. tril 132.56. 

Pamoja na hayo imebainika kuwa uongezwaji wa leseni kinyume cha sheria ambapo imedaiwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Sospeter Muhongo ndio waliohusika na uongezaji wa muda kwenye uchimbaji wa madini.

Kamati hiyo imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kuchukua sheria juu ya kampuni ya ACACIA iliyopo nchini kinyume cha sheria kupitia msajili wa makampuni ikiwa ni pamoja na Mawaziri wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine juu ya mikataba ya uchimbaji madini huku ikiitaka Serikali iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye makampuni ya madini.

Mara 
mara baada ya kukabidhiwa ripotiRais John Magufuli 
ameyakubali mapendekezo yote ya kamati kwa asilimia 100,wahusika wote waliotajwa(Chenge,Ngeleja,Muhongo,Kafumu n.k) wafuatiliwe na vyombo vya dola.

Aidha ameagiza Acacia waitwe na kufanya majadiliano mapya na kuanza usajili upya,kwa sasa Acacia wasisafirishe Makinikia na wataalam wa sheria kupitia wizara ya sheria na katiba ikaunde timu ya wanasheria na kuzipitia sheria zote na zipelekewe bungeni na kupitiwa upya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments