REAL MADRID YATWAA UBINGWA WA UEFA KWA KUWACHAPA JUVENTUS BILA HURUMA



Mechi ilianza kwa kusuasua huku kila upande ukicheza kwa tahadhali kubwa ili wasiruhusu goli lake kuguswa. Juventus wakianza mechi kwa kuonesha ubora zaidi kwenye upande wa Ulinzi ambao uliongozwa na wakongwe kuzuia mashambulizi ya Real, Haikumchukua muda mrefu nyota Christiano Ronaldo aliipatia goli la kuongoza lakini baadae mshambulizi Mario Mandžukić akaisawazishia Juventus na kufanya mchezo kuwa 1 – 1.

Mpaka kipenga kinapulizwa kuashiria mapumziko timu zilikuwa sare kwa goli 1 – 1 huku Real Madrid wakiwa wamemiliki mpira kwa 54% na Juventus 46%.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku pande zote mbili zikijitahidi kushambulia, Dakika ya 61 Casemiro akaiandikia Real goli la pili, Haikuchukua muda mrefu Christiano Ronaldo akaipatia Real goli la 3 dakika ya 65 na kufanya mchezo kuwa 3 – 1 huku Golikipa wa Juventus akionekana kukata tamaa baada ya kufugwa magoli ya haraka haraka ambayo yalimpotezea ramani nzima ya mchezo.


Kosa kubwa walilolifanya Juventus ni kumruhusu Marcelo kuanza kutembea na kutengeneza nafasi ambapo alipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Luka Modrich ambao ulizaa matokeo chanya.


Dakika ya 83 Juan Cuadrado akioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu beki wa Real Madrid Sergio Lamos na kutolewa nge hivyo Juventus kusalia na wachezaji 10.

Goli la 4 la Real Madrid lilipachikwa na Marco Asensio na kufanya mchezo kumalizika Real Madrid 4 huku Juventus 1 na hivyo Real Madrid kutwaa ubingwa wa UEFA Champions League 2016/17.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments