RAIS MAGUFULI KUZINDUA VIWANDA VITANO PWANI


RAIS John Magufuli leo anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Pwani na anatarajia kuzindua viwanda vitano.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua viwanda vikubwa vitano ambavyo ni kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd) na kiwanda cha matrekta (Ursus-TAMCO Co. Ltd) Pia atazindua kiwanda cha chuma (Kiluwa Steel Group), kiwanda cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na atafungua kiwanda cha vinywaji baridi (Sayona Fruits). Pamoja na hayo, pia atazindua mradi wa maji wa Ruvu pamoja na barabara ya Bagamoyo – Msata. Aidha, katika ziara hiyo Rais atakutana n

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments