Picha: DC SHINYANGA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA DIDIA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Alhamis June 15,2017 amefanya ziara katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini na kukagua miradi ya maendeleo. 

Mbali na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia. 

Matiro alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Bakari Kasinyo. 


Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa ziara yake leo Alhamis June 15,2017 katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la Kituo cha Polisi Didia ambacho kipo mbioni kukamilika ujenzi wake 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisilikiza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Didia Luhende Masele ambaye alisema ujenzi wa kituo hicho unalenga kuwasogezea karibu wananchi huduma za kipolisi ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika mji wa Didia ambao una wafanya biashara wengi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akiondoka na msafara wake katika kituo cha polisi Didia kuangalia jinsi ujenzi unavyoendelea 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika zahanati ya kijiji cha Didia ambayo inaendelea kujengwa 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo (kulia) akielezea jinsi ujenzi wa zahanati ya Didia ulivyokwama kumalizika kutokana na kukosekana kwa pesa 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiondoka katika zahanati ya kijiji cha Didia 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bomba la maji ya kisima kirefu katika kijiji cha Chembeli.Mradi upo katika kijiji cha Didia na Bukumbi lakini kijiji cha Chembeli kimesaidiwa mabomba mawili kwa ajili ya wananchi hata hivyo changamoto ni kwamba bomba linaloleta maji limekuwa likipasuka mara kwa mara hivyo kusababisha kero kwa wananchi 
Hapa ni katika moja ya eneo ambapo bomba la maji limekuwa likipasuka na wananchi kulazimika kulifunga kwa mapira/kamba za kuvutika.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kwa Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba (wa tano kulia) 
Bomba likiwa limefungwa kwa mapira/kamba za kuvutika baada ya kupasuka hivi karibuni 
Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba akielezea namna inavyotokea bomba la maji lipasuke.Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alimuagiza kufuatilia na kuchukua hatua madhubuti kuhusu tatizo la bomba la maji kupasuka mara kwa mara katika kijiji cha Chembeli 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli ambapo aliwataka kutunza mradi wa maji uliopo katika kijiji hicho sambamba na kuwahamasisha kulima mazao yanayostahili ukame kama vile mtama,uwele badala ya kutegemea mahindi pekee ili kukabilina na njaa 
Wakazi wa kijiji cha Chembeli wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mkazi wa kijiji cha Chembeli akielezea kero zilizopo katika kijiji hicho 
Mkazi wa kijiji cha Chembeli Maria Tungu akielezea kero ya maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya maji katika visima na mto unaounganisha kijiji hicho na kijiji jirani cha Buyubi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Chembeli wakati akielezea kero yake 
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akizungumza katika kijiji cha Chembeli 
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza katika kijiji cha Chembeli 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasili katika kitongoji cha Danduhu kijiji cha Didia ambapo mkazi wa eneo hilo Mashaka Mayala Komanya amejenga nyumba juu ya mradi wa maji 
Nyumba iliyojengwa juu ya mradi wa maji 
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akimweleza mkuu wa wilaya hatua walizozichukua kutokana na mwananchi huyo kujenga nyumba juu ya mradi wa maji ya visima virefu uliopo katika kata hiyo ikiwa ni kukubaliana bomba linalopita katika nyumba hiyo lihamishiwe karibu na barabara kwani halipitishi maji kwa sasa.Masele alisema mwenye nyumba hiyo anadai mradi huo ulipitishwa hapo bila yeye kushirikishwa 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini kuhakikisha taratibu za vikao zinafuatwa kwa kuandika muhtasari wa makubaliano watakayoyafikia ili kupata muafaka kuhusu jengo hilo kujengwa juu ya mradi wa maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo akimpa maelekezo afisa mtendaji wa kijiji cha Didia Shimba Waziri(wa pili kulia) kuhusu nyumba hiyo kujengwa juu ya mradi wa maji. 



Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments