HII HAPA NCHI NYINGINE ILIVYOJADILI UPYA NA BARICK GOLD KUHUSU MKATABA WA MAKINIKIA

SERIKALI ya Jamhuri ya Dominica na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold ya Canada nao walifanya mazungumzo kumaliza mgogoro kuhusu mkataba wa makinikia kama Tanzania.

Habari kutoka Santo Domingo zinasema Rais wa Dominica, Danilo Medina, mwaka 2013 alisema kwamba mkataba huo una hasara kwa nchi hiyo iliyoko eneo la Carribean na kwamba ujumbe wa kampuni ya Barrick umewasili nchini humo ili kufanya majadiliano mapya ya pamoja.


Serikali ilisema kwamba inataka mkataba huo ujadiliwe upya kwa faida ya pande zote mbili.


Mamlaka za ushuru nchini humo zilishikilia kilo 1,264 za makinikia ambazo zilikuwa zisafirishwe kwenda nje na kampuni Barrick. Makinikia hayo yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. Billioni 49 (Dola Millioni 22 za Marekani) yalikamatwa kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Las Americas, mashariki mwa jiji la Santo Domingo.


Dominica imekuwa ikiishutumu Barrick kwa kufanya udanganyifu wakati wa kujaza fomu za usafirishaji wa vitu mbalimbali nje ya nchi.


Kwa upande wake, kampuni hiyo ya Canada imesema imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Dominica kwa kufuata taratibu zote ambazo bidhaa zote zimekuwa zikikaguliwa na kupitishwa na mamlaka husika za ushuru.


Kampuni hiyo inaendesha shughuli zake katika mgodi wa dhahabu wa Pueblo Viejo katika mji wa Cotui, moja ya migodi mikubwa zaidi duniani ya dhahabu. Kampuni hiyo inamiliki asilimia 60 ya mradi huo na ndiyo inaendesha shughuli zote katika mgodi huo ambapo uzalishaji wa kibiashara ulianza Januari 2013. Kampuni la Goldcorp la Canada linamiliki asilimia 40 ya hisa zilizobaki.


Mnamo Machi mwaka huu, mamlaka za ushuru zilisimamisha usafirishaji wa makinikia wa Barrick kwenda nchi za nje kutokana na madai ya kuvunja taratibu za ushuru.  Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Medina kudai hadharani kwamba kampuni hiyo lazima ifanye majadiliano mapya kuhusu mgodi wa Pueblo Viejo ambao ulikuwa hauendani na maslahi ya nchi hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments