YANGA BINGWA 99% LIGI KUU TANZANIA BARA 2016 / 2017

Shabiki wa Yanga akifurahia ushindi
Ushindi wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans unaifanya Yanga kuusogelea bingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 68 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.

Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya ligi kumalizika, Simba inahitaji kushinda mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa idadi kubwa ya magoli halafu Mbao nayo iifunge Yanga kwa idadi kubwa ya magoli ili Simba itwae taji la VPL kitu ambacho ni kigumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa.

Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata ushindi dhidi ya Toto kwa sababu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikua hazijafungana. Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amis Tambwe dakika ya 81 ya mchezo.

Ikiwa Yanga watalitwaa taji la ligi msimu huu itakuwa ni mara yao ya tatu mfululizo kulibeba taju hilo kuanzia msimu wa 2014-15, 2015-16 na msimu huu 2016-17.

Toto wanaendelea kubaki kwenye hatari ya kushuka daraja wakiwa nafasi ya 15 kwa pointi zao 29 wakiwa wamebakiza mechi moja dhidi ya Mtibwa Sugar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527