WAPIGANAJI WA ALSHABAB WAMUUA MZINZI ALIYEHONDOMOLA TENDO LA NDOA NA MWANAMKE ASIYE WAKE

Wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia wamempiga mtu mmoja na kumuuwa mara tu baada ya kuhukumiwa na mahakama ya kiislamu kwa kosa la uzinzi.

Dayow Mohamed Hassan mwenye umri wa miaka 44 aliuawa kwa kunyongwa na kushambuliwa kwa mawe na wapiganaji wa Alshabab.
Hassan alishtakiwa kwa kosa la kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye sio mke wake na kumpa mimba huku akiwa na wake wawili wa ndoa.
Wapiganaji wa kiislamu wa Alshabab, wamekuwa wakitoa adhabu za aina hiyo mara kwa mara ili kukomesha uzinifu nchini Somalia.
Mwaka 2014, kijana mdogo alipigwa mawe mpaka kufa baada ya kukutwa na kosa la kubaka.
Miaka 4 baadae, msichana mdogo aliuwawa mara baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuwa mzinzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527