SHIRIKA LA AGPAHI LAFUNGA KAMBI YA WIKI MOJA YA WATOTO KUTOKA MARA,SIMIYU NA TANGA JIJINI MWANZA

Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele akitoa hotuba katika sherehe za kufunga kambi ya watoto jijini Mwanza. 
****

SHIRIKA lisilo la kiserikali la AGPAHI limewasihi watoto kuzingatia masomo, kanuni za afya kama zinavyoelekezwa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja kuwahamasisha watoto wengine kujiunga katika vikundi vya watoto.

Rai hiyo imetolewa leo na Meneja wa kanda wa Shirika hilo Dkt. Nkingwa Mabelele wakati wa kufunga kambi ya watoto iliyoandaliwa na shirika hilo iliyojumuisha watoto kutoka mkoa wa Mara, Simiyu na Tanga wenye umri kati ya miaka 9 mpaka 17.

Dkt. Mabelele alisema elimu ni msingi kwa kila mtoto hivyo watoto wanatakiwa kusoma kwa bidii na kuzingatia yale wanayofundishwa ikiwa ni pamoja na kufuatilia kanuni za Afya wawapo shuleni na nyumbani.

Dkt. Mabelele alibainisha kuwa ,Shirika la AGPAHI limeendelea kutoa huduma za kisaikolojia kwa kupitia vikundi vya watoto na kwamba vikundi hivyo vipo katika vituo vya kutolea huduma za Afya za CTC.

Awali katika risala yao, watoto hao walilishukuru Shirika la AGPAHI kwa kuwaandalia kambi hiyo kwani imewasaidia kujifunza mambo mengi ya afya, makuzi, lishe, usafi binafsi pamoja na kufahamiana.

Aidha wameiomba serikali iliunge mkono shirika la AGPAHI ili huduma za kisaikolojia kwa watoto kwa kupitia vikundi ziendelezwe na kuwafikia watoto wengi nchini.

Kwa upande wake, msaikolojia aliyekuwa na watoto kambini kwa muda wa wiki moja amewataka wazazi kuwasikiliza watoto na siyo kuwapiga na kuwatukana kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha watoto wajisikie wanyonge na wasiothaminiwa.

Shirika la AGPAHI lilianzishwa mwaka 2011, hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu shirika limefanikiwa kuwafikia jumla ya watu 189,806 kupata huduma za VVU/Ukimwi ikiwemo kupata dawa za kupunguza makali ya VVU (ARV) na kati ya hao watoto wakiwa 8,615 sawa na asilimia 5%. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA
Watoto wakiwa na Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele wakikata keki
Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele akimlisha keki mmoja wa watoto kutoka mkoa wa Tanga
Watoto wakionesha mavazi ya ubunifu waliyotengeneza kwa kutumia magazeti
Baadhi ya watoto wakiwa na watumishi wa afya walioambatana nao kutoka mikoani wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi hayupo pichani. 
Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele akiwagawia zawadi ya mabegi watoto wote waliokuwa katika kambi hiyo
Utoaji wa zawadi ukiendelea kwa watoto wote 50 waliohudhuria katika kambi hiyo 
Meneja Mawasiliano na Uragbishi wa shirika la AGPAHI Tanzania Jane Shuma akitoa ufafanuzi wa kukabidhi vyeti kwa watumishi wa afya.
Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele akitoa zawadi na cheti kwa mtumishi wa afya aliyeambatana na watoto kutoka Mara.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea katika sherehe ya kufunga kambi ya watoto iliyofanyika katika ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza. 
Dkt. Maimuna Ahmed, aliyekuwa anawahudumia watoto katika kipindi cha kambi akiwaasa watoto hao kuzingatia maelekezo ya wahudumu wa afya.
Watoto kutoka Simiyu,Tanga na Mara waliohudhuria katika kambi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi na Meneja wa shirika la AGPAHI kanda ya Ziwa Victoria,Dkt. Nkingwa Mabelele 
Watoto kutoka Simiyu,Tanga na Mara waliohudhuria katika kambi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa afya na wanasaikolojia waliokuwa katika kambi hiyo.

Picha ya pamoja baada ya kufunga rasmi kwa kambi ya watoto leo katika viwanja vya shule ya Nyakahoja jijini Mwanza.

Picha zote kwa hisani ya Kijukuu blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527