RAIS MAGUFULI AKABIDHI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI - EAC KWA RAIS MUSEVENI

Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.

Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.

“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.

Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.
“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.

Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527