JTFE YATOA MSAADA KITUO WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA NA WADIAKONIA KKKT -DKMZV


Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) inayojishughulisha na masuala ya watu wenye Ualbino leo Ijumaa May 26,2017 imetoa msaada wa miwani ya kuzuia mionzi ya jua,viatu, vifaa vya michezo kwa watoto ikiwemo midoli katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga chenye watoto wenye ualbino 142,wasioona 26 na wasiosikia 60.

Mbali na kutoa vifaa hivyo katika kituo cha Buhangija pia JTFE imetoa msaada wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua na miwani ya kuzuia mionzi ya jua katika Kituo cha Wadiakonia cha Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria kilichopo Mwasele katika manispaa ya Shinyanga.

Akuzungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa JTFE yenye makao makuu yake nchini Uholanzi, Pieter Staadegaard alisema wametoa msaada huo ili kuonesha kuwa wanawajali watoto hao na kwamba wao ni kama watu wengine katika jamii.

“Huko Uholanzi naishi na watoto watatu kati yao mmoja na ualbino,nilipowaambia ninakuja Tanzania,wakanipatia zawadi hii ya vifaa kwa ajili ya watoto ikiwemo hii midoli kwa ajili ya watoto wenzao wa hapa Buhangija”,alieleza Staadegaard.

Aidha aliitaka jamii kuwathamini na kuwapenda watu wenye ualbino badala ya kuwafanyia ukatili kwani ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.

Staadegaard alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi JTFE,Josephat Torner na viongozi wa Idara ya wanawake na watoto na diakonia kutoka kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria 

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kituo cha Buhangija na Wadiakonia 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi JTFE,Josephat Torner katika kituo cha kulelea watoto cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akimpa midoli Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi JTFE,Josephat Torner kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akizungumza wakati wa kupokea zawadi hiyo
Zoezi la kugawa zawadi kwa watoto likiendelea
Watoto wanapokea zawadi.Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Wanawake na Watoto kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Edna Shoo
Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akigawa midoli kwa watoto
Watoto wakiwa katika foleni kwa ajili ya zawadi
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akimvalisha miwani ya kupunguza mionzi ya jua mmoja wa watoto waliopo katika kituo cha Buhangija
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard  akiwa na mtoto mwenye ualbino mara baada ya kumvalisha miwani
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard  akiwa na mtoto mwenye ualbino
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard  akimvalisha viatu mtoto mwenye ualbino
Mtoto akivaa viatu,zawadi kutoka JTFE
Watoto wakiendelea kuvaa viatu
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard   akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino baada ya kuwapa zawadi ya viatu
Hapa ni katika kituo cha Wadiakonia kanisa la KKKT-DKMZV ,Pichani  ni mkurugenzi wa idara ya wanawake,watoto na diakonia kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ambarang'u akimkaribisha  Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard katika kituo hicho
Mkurugenzi wa idara ya wanawake,watoto na diakonia kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ambarang'u akielezea kuhusu kituo hicho ambacho kinalea vijana wa kike wenye ualbino kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ikiwemo kushona nguo kwa kutumia cherehani.Wa Kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza katika kituo hicho na kuwataka vijana hao kuzingatia ujuzi wanaopatiwa ambao utawasaidia katika maisha yao na waweze kusaidia pia watu wengine
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akimvalisha miwani mmoja wa vijana hao.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE)Josephat Torner
Vijana hao wakiwa wamevaa miwani ya kupunguza mionzi ya jua
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akigawa mafuta yanayopunguza mionzi ya jua
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiendelea kugawa mafuta
Zoezi la kugawa tisheti zilizotolewa na kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria likiendelea
Mratibu wa Diakonia kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Matrida Sanga akimwonesha Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard kazi zinazofanywa na vijana hao
Viongozi wa JTFE na vijana wanaolelewa katika nyumba ya wadiakonia 
Picha ya pamoja,viongozi wa JTFE,viongozi wa Idara ya wanawake na watoto na diakonia kutoka kanisa la  KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria na vijana waliopo katika kituo hicho
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527