POLISI DAR YAMKAMATA KIJANA ALIYECHINJA MPENZI WAKE NA KUMUWEKA KWENYE DIABA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika diaba/jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.


Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.


Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;


“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.


Sirro ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527