Picha 45:TAMASHA LA KUIMBA NA KUABUDU VIJANA KANISA LA TAG SHIYANGA UWANJA WA SHYCOM SIKUKUU YA PASAKA



Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Shinyanga limeadhimishisha sikukuu ya pasaka kwa kufanya tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga.

Kongamano hilo limeandaliwa na kanisa la TAG Shinyanga kupitia idara ya Mabalozi wa Yesu “ Christ Ambassadors – CA’s) ambapo awali vijana wa kanisa la TAG Shinyanga walianza kwa maandamano kuanzia katika kanisa hilo lililopo eneo la Moleka mjini Shinyanga kisha kuelekea katika uwanja wa Shycom. 

Mkurugenzi wa idara ya mabalozi wa Yesu kanisa la TAG jimbo la Shinyanga Mchungaji Seleman Joseph alisema katika kuadhimisha siku ya kufa na kufufuka kwa Yesu kristo wameandaa tamasha la kumsifu na kumwabudu mungu ili watu wamrudie mungu na kuacha vitendo viovu.

Alisema mabalozi hao wa yesu wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa Jamhuri ya muungano Dkt. John Pombe Magufuli katika kupiga vita vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.



Vikundi mbalimbali vya uimbaji vilishiriki katika tamasha hilo la uimbaji huku Mchungaji Gabriel Sondole kutoka kanisa la TAG Penueli Ndembezi Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa kipindi cha kuabudu.


Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo katika Tamasha hilo ametuletea picha 45 za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo mpaka mwisho saa tisa alasiri mpaka saa moja usiku Jumapili Aprili 16,2017
Maandamano yalianzia kanisani-Pichani ni vijana wa kanisa la TAG wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali
Vijana Mabalozi wa Yesu kanisa la TAG jimbo la Shinyanga wakitoka eneo la kanisa hilo kuelekea uwanja wa Shycom
Vijana wakiwa katika maandamano 
Kijana Emmanuel Hezron akiigiza kama Yesu msalabani 
Waandamanaji wakipita mjini Shinyanga 
Maandamano yanaendelea 
Vijana wakiwa wameshikilia mabango wakati wa maandamano hayo 
Maandamano yanaendelea
Kijana aliyeigiza Yesu akiwa msalabani akiwa kwenye maandamano kuelekea uwanja wa Shinyanga
Maandamano yanaendelea
Maandamano yanaendelea
Kijana Emmanuel Hezron kutoka Ngokolo Shinyanga aliyeigiza Yesu msalabani akiwa katika uwanja wa Shycom mjini Shinyanga ambapo tamasha la kuimba na kuabudu limefanyika
Vijana wakiwa na mabango katika uwanja wa Shycom
Mkurugenzi wa idara ya mabalozi wa Yesu kanisa la TAG jimbo la Shinyanga Mchungaji Seleman Joseph akizungumza kwenye tamasha la kumsifu na kumwabudu mungu ili watu wamrudie mungu na kuacha vitendo viovu
Mkurugenzi wa idara ya mabalozi wa Yesu kanisa la TAG jimbo la Shinyanga Mchungaji Seleman Joseph akizungumza katika uwanja wa Shycom 
Katibu wa kanisa la TAG Shinyanga,mchungaji Baraka Laizer akimkaribisha Askofu mstaafu wa kanisa la TAG Shinyanga Yehoshephat Masaga ili afungue rasmi Tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom
Viongozi wa kanisa la TAG Shinyanga wakiwa katika uwanja wa Shycom
Katibu wa kanisa la TAG Shinyanga,mchungaji Baraka Laizer akimkaribisha Askofu mstaafu wa kanisa la TAG Shinyanga Yehoshephat Masaga kwa ajili ya ufunguzi wa tamasha hilo
Askofu mstaafu wa kanisa la TAG Shinyanga Yehoshephat Masaga akifungua tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom
Askofu mstaafu wa kanisa la TAG Shinyanga Yehoshephat Masaga akifungua tamasha hilo
Vijana wa kanisa la TAG wakiwa katika uwanja wa Shycom
Kundi la uimbaji wa nyimbo za sifa na kuabudu katika kanisa la TAG Shinyanga wakiwa uwanjani
Vijana wakicheza uwanjani
Vijana wakicheza uwanjani
Tamasha linaendelea
Askofu Josephat Mussa wa kanisa la Tanzania Mision Revival Church (TMRC) akiomba wakati wa tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom mjini Shinyanga
Vijana wakiomba uwanjani
Mchungaji Gabriel Sondole kutoka kanisa la TAG Penueli Ndembezi Shinyanga akitoa mahubiri wakati wa tamasha la kuimba na kuabudu katika uwanja wa Shycom 
Mchungaji Gabriel Sondole akiendelea na mahubiri
Mwalimu wa Injili Happiness Kihama Mwaja akifuatilia mahubiri
Mchungaji Gabriel Sondole akiwaombea wakazi wa Shinyanga waliomua kuokoka na kumrudia mwenyezi Mungu
Mchungaji Gabriel Sondole na Mkurugenzi wa idara ya mabalozi wa Yesu kanisa la TAG jimbo la Shinyanga Mchungaji Seleman Joseph
Maombi yanaendelea
Maombi yanaendelea
Tunafuatilia yanayojiri uwanjani....
Kijana Emmanuel Hezron akiigiza kama Yesu msalabani wakati wa maandamano ya vijana kutoka kanisa la TAG Shinyanga akiwa katika uwanja wa Shycom
Kushoto ni Muimbaji Scola akiimba jukwaani
Vikundi vya uimbaji vikiendelea kuimba
Mwalimu wa Injili Happiness Kihama Mwaja akiimba jukwaani
Mtoto akisali wakati Mwalimu wa Injili Happiness Kihama Mwaja akiimba jukwaani
Uimbaji unaendelea
Vijana wakicheza
Vijana wanacheza na kuimba
Vijana wanacheza jukwaani
Vijana wanaruka jukwaani



Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527