KIKWETE: NI ZAMU YANGU KUMUUNGA MKONO MKE WANGU...

Baada ya kupokelewa kwa shangwe katika ukumbi wa bunge leo hii, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amesema ni zamu yake kwa sasa kumuunga mkono mkewe Mama Salma Kikwete.

Kikwete aliyekuwa ameambatana na familia yake, ameshuhudia mkewe akila kiapo cha ubunge katika kikao cha kwanza cha bunge lililoanza leo mjini Dodoma.

Salma Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa WAMA, alionekana kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mumewe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kulitumikia taifa.

“Leo asubuhi nmeshuhudia kiapo cha mke wangu, mheshimiwa Salma Rashd Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga mkono,”alinukuliwa Kikwete katika akaunti yake ya twiter.

Kikwete aliingia ndani ya bunge hilo huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.
View image on TwitterView image on Twitter
Leo asubuhi nimeshuhudia kiapo cha Mke wangu Mhe. Salma Rashid Kikwete kuwa Mbunge wa Kuteuliwa Bungeni Dodoma.Ni zamu yangu kumuunga mkono.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527