KAULI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA KUPOTEA KWA ROMA MKATOLIKI

Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni, Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.


“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527