DIAMOND PLATNUMZ AMPIGIA MAGOTI ASKOFU GWAJIMA BAADA YA KUMVURUGA KWA WIMBO WAKE MPYA

Hazijafika saa 72 toka mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz aachie wimbo mpya ambao unagusia yanayoendelea sasa hivi Tanzania ambapo baada ya Askofu Gwajima kuusikia, alitumia time yake kupost kwenye Instagram yake haya maneno hapa chini.

Baada ya Diamond Platnumz kuona post hiyo ya Askofu Gwajima ameyaandika yafuatayo >>> “Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima
“Nilisema: mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mrefu wangekaa chini na kumaliza na wote kufurahi kwa pamoja
“Lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikuwa anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi? chondechonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆😅

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527