Picha: MKUTANO WA WADAU WA MKONGE WILAYA YA KISHAPU - SHINYANGA NA MEATU - SIMIYU


Alhamis ,Machi 16,2017 kumefanyika Mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu na wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.



Mgeni rasmi katika mkutano huo ulioandaliwa na shirika la OXFAM na asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na Maendeleo ya Jamii (Relief to Development Society- REDESO) alikuwa mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba.


Awali akizungumza katika mkutano huo,Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele alisema lengo la mkutano huo kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kufahamiana sambamba na kujadili namna ya kulifanya zao hilo kuwa na tija na manufaa zaidi kwa wakulima na kuwasaidia wakulima hao kupata masoko.

"Tumekutana hapa ili tujadili pia namna ya kumuunganisha mkulima wa mkonge anufaike na masoko yenye  faida na kupata uwakilishi mzuri katika sekta hii",alisema Kihwele.

Akizungumza katika mkutano huo,mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba aliwataka wadau wa zao la mkonge kwenda kuwekeza kwa kujenga viwanda katika wilaya yake kwani ardhi ipo ya kutosha.

"Wadau wa mkonge njooni Kishapu muwekeze,tunayo ardhi ya kutosha,hivi sasa maji kutoka ziwa Victoria yamefika Kishapu,umeme na barabara zinazopitika kipindi chote zipo,tunataka kulifanya zao la mkonge kuwa rasmi badala ya kutumika kwenye mipaka kutenganisha mashamba na milingoti kwa ajili ya kujengea nyumba",alieleza Nyabaganga.

"Kipindi cha majaribio kimekwisha,tunalima pamba lakini pia tumeamua kulima mkonge,tunataka kilimo hiki kiwe rasmi,wananchi wanajitahidi kulima zao la mkonge lakini changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa soko hivyo ni vyema ofisi za bodi ya mkonge zikawa na ofisi katika maeneo yanayolima,wakulima wanahitaji kunyanyuliwa kwani hata mikopo inayotolewa haitoshi",aliongeza Nyabaganga.

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika mkutano huo ni wakulima na wasindikaji wa zao la mkonge,wazalishaji wa bidhaa za mkonge,taasisi za kifedha ikiwemo Vision Fund,bodi ya mkonge (TSB),Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA),Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO),Umoja wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA),Mtandao wa Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors Forum -ANSAF) na viongozi mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Meatu.

Tazama picha 26 za matukio yaliyojiri wakati wa mkutano huo
Mratibu Miradi (uchumi) kutoka shirika la OXFAM Haji Kihwele akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa zao la mkonge uliofanyika katika ukumbi wa Virgimark Hotel mjini Shinyanga leo Alhamis Machi 16,2017-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Wadau wa zao la mkonge wakimsikiliza Mratibu Miradi Kiuchumi kutoka OXFAM Haji Kihwele
Meneja Mradi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na maendeleo ya jamii (Relief to Development Society- REDESO) Charles Buregeya akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutok wilaya ya Kishapu na Meatu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa mkutano huo
Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mheshimiwa Nyabaganga Talaba akizungumza ukumbini ambapo alisema serikali imedhamiria kuanzisha viwanda na kwamba kinachotakiwa ni kuwa tayari kuzalisha zao la mkonge.Kulia ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu George Kessy
Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na Afisa Biashara halmashauri ya wilaya ya Kishapu Konisaga Mwafongo
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akisisitiza jambo kwenye mkutano huo
Meneja Mradi REDESO Charles Buregeya (kushoto) na Mratibu Miradi (uchumi) shirika la OXFAM Haji Kihwele
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akizungumza ukumbini
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa zao la mkonge
Mwakilishi wa Shirikisho la Wakulima na Wasindikaji wa zao la mkonge wilaya ya Kishapu( SHIWAKI),Yusuph Mboje akielezea kuhusu kazi zinazofanywa na shirikisho hilo lililoanzishwa mwaka 2016 ambalo linakabiliwa na changamoto ya kukosa soko la mkonge na kukosekana kwa mkataba na mnunuzi wa kudumu wa zao hilo
Mwakilishi wa akina mama wanaojishughulisha na kilimo cha mkonge Anastazia Christopher kutoka Kishapu akielezea faida wanazozipata kupitia kilimo cha mkonge ambazo ni pamoja kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao,kusomesha watoto n.k
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo na mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba wakiwa ukumbini
Mratibu wa Miradi (Ardhi) kutoka OXFAM bi Amina Ndiko akiongezea maelezo kutoka kwa akina mama kutoka Kishapu wanaolima mkonge
Mkulima wa zao la mkonge kutoka Kishapu Fredina Said akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Nyabaganga Talaba zulia lililotengenezwa kwa mkonge
Mraghbishi kutoka Taasisi ya Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora (ADLG) ambaye pia ni Mwakilishi wa Mtandao wa Asasi za Wakulima (Agriculture Non- State Actors Forum -ANSAF) bwana Nicholaus Luhende Ngelela akizungumza kwenye mkutano huo ambapo alisisitiza umuhimu wa wakulima wa zao la mkonge kuunda mtandao wao 
Katibu mtendaji Chemba ya wafanyabiashara,wakulima na viwanda (TTCIA) mkoa wa Mwanza Hassan Karambi akizungumza ukumbini
Taasisi isiyo ya kiserikali yenye kusaidia sekta ya kilimo (Private Agricultural Sector Support - PASS) Emilian Barongo akizungumza ukumbini 
Jeremiah Maleko kutoka Vision Fund akieleza namna wanavyotoa mikopo kwa wakulima


Afisa udhibiti Ubora kutoka Bodi  ya Mkonge Olivo Mtunge akielezea kuhusu hali ya soko la mkonge hivi sasa  na fursa za mkulima mdogo ili aweze kunufaika na kilimo hicho


Picha ya pamoja washiriki wa mkutano wa wadau wa zao la mkonge kutoka wilaya ya Meatu na Kishapu

Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527