STEVE NYERERE AKIRI KUWA SAUTI INAYOSAMBAA MTANDAONI NI YAKE..AKERWA NA MAMA WEMA SEPETU KUMREKODI

Baada ya sauti zilizosambaa zikimuhusisha Mwigizaji Steve Nyerere na Mama wa mwigizaji Wema Sepetu wakizungumza huku akitaja baadhi ya viongozi mbalimbali aliodili nao kwenye sakata la Wema kushikwa na Polisi, leo Steve Nyerere ameita Waandishi wa habari na kuongea nao.

Steve Nyerere amesema kuwa hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.

Amesema katika wasanii mbalimbali ambao huenda walilipwa pesa nyingi zaidi ni Wema Sepetu pamoja na yeye na kusema wao pamoja na wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya 'Mama ongea na mwanao' ni wasanii ambao walilipwa vizuri sana na Chama Cha Mapinduzi kuliko wasanii wengine wowote wale.

Steve Nyerere anasema katika mkataba walioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi  chama hicho kitakuja kukusaidia. 

Pia Steve Nyerere anakiri wazi kuwa sauti ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ni sauti yake na alikuwa akiongea vile ili kumridhisha mama yake na Wema Sepetu kwani wakati huo jambo hilo lilikuwa ngumu kwake. 

==> Fuatilia maongezi yake ya moja kwa moja hapo chini
 
1.Nimewaiteni hapa kama msanii wa tasnia ya filamu pia kama kada wa chama cha mapinduzi

2.Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe

3.Nilichofanya ni kutumia sanaa yangu na ujuzi kumtoa mama kwenye hali ambayo anasema anataka kujitoa hata kwenye chama"

4.Mama alikuwa anaamini naweza kumtoa Wema, nilikuwa natumia ujuzi wa akili yangu kumlidhisha mama, kumbe yeye ananirekodi

5.Kwenye kampeni tulilipwa hakuna aliyefanya kazi bila kulipwa, kundi la mama ongea na mwanao mimi ndio nilikuwa mwenyekiti

6.Maneno niliyoyasema ktk simu na Mama Wema na kutaja viongozi ni UONGO, ilibidi nifanye hivyo maana sikuwa na jinsi...

7.Uwezo wa kuwaambia Wabunge au kuwaelekeza cha kufanya sina, sina ujanja huo.... namuomba radhi Spika Job Ndugai" 

8.Mimi na Wema ndio tuliwafuata CCM kwamba tuna wazo la mama ongea na mwanao, na tukalipwa

9.Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza

10.Nia yangu haikua mbaya, wakati naongea na Mama niliamini ni mama mzazi... ile audio ina siku 5, kwanini iachiwe juzi?

11.fikifria ile audio ina siku tano, inakuja kutolewa juzi na watu wamehama tayari chama, nafikiri walifanya hivyo kunichafua

12.Ile audio imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi

13.Nimetaja viongozi ktk ile audio alafu unakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya kuisambaza ni mauaji

14.Si kweli nilishinkiza wabunge wamjadili Wema, mtoto anapotaka kuchomwa Sindano kuna vitu anaambiwa, ndio hivyo nilivifanya

15.Watanzania wenzangu usimuamini binadamu yeyote, Mama Wema alitaka kuniharibia maisha yangu, Mama kanikosea.. namuachia Mungu

16.Mimi na Makonda hatujawahi kwenda alikokutaja Mama, ilibidi niitikie kama zoba, Waandishi naomba mkaseme NAOMBA RADHIII

17.Sina ugomvi na Makonda na ninamuomba msamaha na hakuna ukweli kwamba siongei nae.... Paul ni kaka yangu, tunawasiliana

18.Naliomba radhi bunge tukufu na Spika Ndugai kwa kauli ya kusema nimeshinikiza bunge, nilifanya hivyo kutaka asitoke ndani ya CCM

19.Uwezo wa kuwashinikiza wabunge sina na wala mamlaka hiyo sina

20.Hii kesi kila mtu alirudi nyuma.. ni maulizo tu inaendeleaje? tunamuombea kwa Mungu tu, CCM ni kama bahari wametoka wangapi?

21.Mimi kama mtu wa karibu na familia nilitakiwa nitoe maneno matamu na ndio hayo

22.Kwenye project ya kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 MAMA ONGEA NA MWANAO hatuidai CCM hata senti tano

23.Alichofanya mama kunirekodi huo ni uuaji, kuna watu wananitegema nyuma ya Steve alitaka anigombanishe na marafiki

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527