Makubwa Haya!! NJIWA ATUMWA KUPELEKA SIMU KWA MFUNGWA GEREZANI

Brazil inatajwa kuwa nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya Wafungwa gerezani ambapo ina Wafungwa 600,000 kwenye magereza yake na kama unakumbuka hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kihalifu ndani ya Magereza na yamesababisha vifo vya wafungwa 140.

Sasa kingine kilichoripotiwa ni kutokea kwenye gereza la Franco da Rocha ambapo Njiwa amekamatwa na Askari akipeleka simu ya mkononi kwa mfungwa ambapo bado haijafahamika aliyekuwa akimtumia Ndege huyo kupeleka simu.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza lakini hayajajibiwa…. Njiwa huyo alielekezwa vipi? akili gani imetumika kumuongoza? alikua anatumia njia gani kuikabidhi simu?

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527