Audio: WATUHUMIWA 17 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA SHINYANGA...MAJINA MENGINE ZAIDI YA 20 YAPO KWA DC SHINYANGA


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo (hawapo pichani) Alhamis Februari 9,2017 kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya katika wilaya ya Shinyanga-Picha na Kadama  Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akielezea jinsi wananchi wa wilaya hiyo waliamua kuchukua hatua ya kupeleka majina ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wilayani humo
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akielezea kuhusu kikosi kasi walichounda kufuatilia majina ya watu wanaotajwa kuhusika na dawa za kulevya wilayani humo


******
Vita dhidi ya dawa za kulevya imetua mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu 17 wanaotuhumiwa kuwa ni watumiaji wa dawa hizo ikiwemo unga na mirungi wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17 kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya. 

“Mheshimiwa rais ametangaza kuwa hii ni vita ya nchi nzima,baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya ikiendelea mkoani Dar es salaam,wametuletea majina zaidi ya 20 ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya,wanasema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa hizi”,amesema Matiro. 

“Wananchi wenyewe kwa moyo mweupe kabisa ndiyo wametuletea majina ya watu wanaotumia na kuuza dawa za kulevya ikiwemo unga na mirungi,kamati ya ulinzi na usalama tumeunda kikosi kazi cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya”,alisema Matiro. 

Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi kwa jitihada zake dhidi ya dawa za kulevya na kufanikisha kukamata watuhumiwa 17 huku akikisisitiza kuwa vita hiyo siyo ya Dar es salaam pekee bali inatakiwa kufanyika nchi nzima kwani watumiaji na wauzaji wa dawa hizo wapo kila mahali nchini. 

Msikilize hapa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia watuhumiwa wa dawa za kulevya wilayani Shinyanga.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527