ATUPWA JELA MIAKA MITATU KUWA KUJIOZESHA MWANAFUNZI WA MIAKA 14


HAKIMU wa Mahakama ya Wilaya ya Kusini Makunduchi, Zanzibar, Ali Abrahman amemhukumu Khatib Mohammed Khatib (57), kwenda jela miaka mitatu, baada ya kupatikana na kosa la kumtorosha msichana wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa shule.

Pamoja na kutupwa jela pia ametakiwa kulipa fidia ya Sh 500,000, ambapo endapo atashindwa kulipa atalazimika kutumikia miezi sita jela.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Abrahman alisema mahakama imeridhika na ushahidi wa mashahidi saba waliofika mahakamani hapo wakiwemo watatu kutoka kwa watetezi wa kesi na watatu kutoka kwa mshitakiwa.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 22 mwaka 2016 huko Nganani Makunduchi, kwa kumtorosha na kumpeleka Bondeni mtoto wa miaka 14, bila ya idhini ya wazazi wake.






Mapema Mwendesha Mashtaka Ali Yussuf aliiomba mahakama kutoa adhabu ambayo itakuwa fundisho kwa wengi wenye tabia hiyo.

Via>>Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527