HUYU NDIYO MISS WORLD 2016...AFRIKA YAINGIA TOP 5


Najua watanzania na waafrika wote walikuwa wanahamu ya kufahamu mshindi wa Miss World 2016 atakuwa ni mrembo kutoka nchi gani, mashindano hayo ambayo yamefanyika Washington Marekani, Afrika ilipata nafasi ya nchi za Kenya na Ghana kuingia TOP 20.



TOP 5 ya Miss World 2016

Muda ulifika na waandaaji wa Miss World walitangaza mshindi ambapo Miss Puerto Rico ndio alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2016, lakini muwakilishi wa TanzaniaDiana Edward kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufika nafasi za juu.

Mshindi wa Miss World 2016

Hata hivyo Afrika Mashariki imepokea good news baada ya nchi ya Kenya kufanikiwa kuingia TOP 5 na ndio nchi pekee ya Afrika iliyofanikiwa kuingia TOP 5, huku Miss Dominician Republic akishika nafasi ya pili na Miss Indonesia akishika nafasi ya tatu.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527