DEREVA MBARONI KWA KUSAKATA MUZIKI AKIENDESHA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo, alimtaja dereva anayeshikiliwa kuwa ni Saidi Juma (26) mkazi wa Dodoma ambaye inadaiwa siku ya tukio alikuwa anaendesha basi aina ya Nissan Civilian lenye namba za usajili T.360 DAY huku akicheza muziki.
Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4, mwaka huu, saa 11: 00 jioni katika Mji Mdogo wa Itigi wilayani Manyoni wakati mtuhumiwa akiwa na wenzake watatu, alipoendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari kwa kucheza muziki huku akiachiana usukani na wenzake hao wakati gari hilo likiwa kwenye mwendo.
Kamanda Towo aliwataja watuhumiwa wengine ambapo pia wanashikiliwa na Polisi kuwa ni Joseph Ramadhan (27), Ezekiel Joseph (24) na Sebastian Godfrey (23) wote wakazi wa Majengo, Itigi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527