Sunday, October 9, 2016

WACHEZAJI WA STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' WALIA NJAA

 
LICHA ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara, wachezaji wa Stand United wanalia njaa kwani hawajalipwa mishahara yao ya miezi mitatu.

Stand ambayo ilianza ligi ikiwa kwenye mgogoro mkubwa wa mgawanyiko wa Asili na Kampuni, kwa sasa ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 16.

Akizungumza na gazeti la Habarileo juzi, kocha mkuu wa timu hiyo Mfaransa Patrick Liewig alisema wachezaji wake hawajalipwa mshahara wa miezi mitatu hivyo anaomba uongozi wa timu hiyo uwalipe.

“Miezi mitatu hawajalipwa, hawa hawahitaji kingine zaidi ya mishahara yao, viongozi wafanye wawalipe,” alisema.

" Baada ya mchezo wetu na timu ya Majimaji, uongozi ulituahidi kuwa tutapata mahitaji yetu yote lakini kwa sasa wanasema hawana pesa," alisema Liewig.

Liewig alisema kwa sasa timu yake ina hali ngumu na kwamba kwa vile wachezaji wake wanacheza kwa kujituma na uvumilivu ndio maana wanapata ushindi. Kocha huyo alilaumu mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi kutaka kufanya hujuma ili wapoteze mechi hiyo.

" Katika mchezo wetu na Majimaji mmoja wa watu wa benchi la ufundi (anamtaja) alijaribu kuwarubuni wachezaji wetu ili tufungwe lakini wachezaji waligoma.

Wachezaji wangu wapo hapa kwa ajili ya kufanya kazi na sio kupokea rushwa. Msimu uliopita wachezaji (anawataja) walikuwa wakifanya hujuma tufungwe lakini safari hii hawapo katika timu yangu na ndio maana unaona tunakwenda vizuri,” alisema.

Kocha Liewig anamtaja mmoja wa viongozi hao wa benchi la ufundi kwamba alihusika kufanya hujuma katika moja ya mechi dhidi ya timu kubwa msimu uliopita ambapo timu yake ilifungwa mabao 4-0.

Chanzo-Habarileo

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde1 blog Inapatikana Play Store…Download HAPA ,Tuwe Tunakutumia Habari Kwenye Simu Yako
 Bofya Hapa
Share:

Tafuta Habari Hapa

Subscribe You Tube Channel Yetu

 Bofya Hapa

Manju Matemba - Beni

DC Shinyanga Josephine Matiro akitema cheche kwa maafisa watendaji

Pakua Videozetu App

Kutana Able wa Michoro

Habari Kuu

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2017,TAREHE YA KURIPOTI KAMBINI

TAARIFA KWA UMMA Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita kwa mwaka...

Classic Visual Shinyanga

Habari Gumzo Mtandaoni

Mshana Computer Solution

Habari Zilizopita

Jiunge Nasi Hapa

Translate This Blog

Copyright © MALUNDE 1 BLOG | Powered by Malunde