STAND UNITED "CHAMA LA WANA"WAICHAPA AZAM FC...ANGALIA HAPA MSIMAMO WA VPL BAADA YA MECHI ZA LEO OKTOBA 12



Mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara zimechezwa leo Jumatano ya Oktoba 12, 2016 katika viwanja tofauti Tanzania, kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans wameshuka dimbani kucheza mchezo wao wa 7 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Uhuru.

Yanga ambao wamekuwa na rekodi ya ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika kipindi cha misimu miwili, wameendeleza rekodi yao kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 45, Simon Msuva dakika ya 68 na Donald Ngoma akitokea benchi dakika ya 80 wakati goli la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo dakika ya 64.


Mara ya mwisho Mtibwa Sugar na Yanga kucheza ilikuwa ni October 6 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, siku ambayo Mtibwa walijaribu kutaka kuondoa uteja ila ikashindikana na kuishia kuambulia suluhu ya 0-0, Yanga ambao wanaonekana kama kupungua kasi kwa mechi zao za karibuni, watakuwa na mtihani Jumapili dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Uhuru pia.



Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo Oktoba 12 2016
Mbeya City 0-2 Simba
Mbao FC 3-1 Toto Africans
Mwadui FC 2-0 African Lyon
Majimaji FC 0-1 Kagera Sugar
JKT Ruvu 0-0 Prisons
Stand United 1-0 Azam FC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527