News Alert!! ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA 2016




Serikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya msingi Kwema ya mkoani Shinyanga.

Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Saba umeongezeka kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati anatangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa Darasa la Saba mwaka 2016.

Amesema, watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu na watajiunga na kidato cha kwanza 2017.

"Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271540. Mwaka 2015 watahiniwa waliofaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwa kuwapo ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” amesema Dk Msonde.
 Watahiniwa 16,929 wamepata daraja A, 141,616 wamepata daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E .

Aidha watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu. 






AU 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527