STAND UNITED "CHAMA LA WANA" WAIBABUA YANGA 1 - 0 ,ANGALIA PICHA

 
Furaha ikiendelea baada ya ushindi



Mchezaji wa Stand United Pastory Athanas aliyeiua Yanga leo

Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea leo Septemba 25 2016 kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya  Dar es Salaam Young Africans kushuka katika uwanja wa CCM Kambarage kucheza na wenyeji wao Stand United katika mchezo wao wa 5 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016.


Stand United ‘Chama la Wana’ wamevunja rekodi ya Yanga baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa leo uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.


Bao pekee la Stand limefungwa na Pastore Athanas ambalo limeifanya tumu take iibuke na pointi tatu kwenye uwanja wa nyumbani.


Licha ya Stand kuwa kwenye mpasuko mkubwa wa kiutawala, timu hiyo bado haijapoteza mchezo wowote kwenye uwanja wao wa nyumbani hadi sasa tangu kuanza kwa ligi mzimu huu 2016-2017.


Rekodi za Yanga zilizovunjwa na Stand United

  • Stand United imeifunga Yanga kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ya Shinyanga mjini ilipopanda daraja.

  • Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa  VPL msimu baada ya kucheza mechi nne bila kufungwa. Mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi ilikuwa 3-1 dhidi ya TP Mazembe nchi DR Congo katika mashindano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi.

  • Stand United imekuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga. Awali Yanga ilikuwa imecheza mechi nne za ligi bila kuruhusu goli huku yenyewe ikiwa imefunga magoli nane. (Yanga 3-0 African Lyon, Ndanda 0-0 Yanga, Yanga 3-0 Maji Maji, Mwadui 0-2 Yanga)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527