Kimenuka!! MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AVURUGWA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI,AWACHANA BILA UOGA..MSIKILIZE HAPA AKIFUNGUKA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack 
*****

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amegeuka mbogo katika kikao cha wadau wa mazingira na kutishia kuwatumbua wakurugenzi wa halmashauri sita za wilaya katika mkoa huo baada ya kushindwa kuhudhuria kikao hicho ambacho kimsingi alidai kilikuwa kinawahusu wao.Anaripoti mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde



Kikao hilo kimefanyika jana Septemba 19,2016 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira wakijadili namna ya kuuondoa mkoa huo katika hali ya jangwa kwa kupanda miti.


Wakati kikao kikiendelea ghafla mkuu huyo wa mkoa alibaini kuwa kikao chake kimepwaya kutokana na wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya katika mkoa huo na baadhi ya watumishi wa serikali kutohudhuria bila kumpa taarifa.(Sikiliza sauti yake hapa chini)


“Haiwezekani niwaalike halafu asitokee hata mmoja,ndugu katibu tawala wa mkoa,nataka wakurugenzi wote waandike maelezo ndani ya masaa 24 kwani hawajahudhuria kikao change,nimeona hapa panapwaya,watu wamechukua likizo bila kutoa taarifa,kama mlizoea hivyo mimi siko hivyo tusije kulaumiana”,aliongeza Mkuu huyo wa mkoa.


“Hiki ni kikao cha kazi lakini wakurugenzi wote hawapo,sitaki mnijaribu,vikao vyangu vyote sitaki kuletewa wawakilishi pasipo na sababu za msingi kwa sababu hawawezi kufikisha ujumbe kama inavyotakiwa,tena nataka yeyote anayealikwa kuhudhuria vikao vyangu afike mwenyewe tena kwa wakati uliopangwa ”,alieleza Telack.



Mkuu huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi wa serikali kuacha kulala badala yake watimize wajibu wao kwani sasa ni muda wa kufanya kazi hakuna kubembelezana na kwamba asiyetaka kufanya kazi aandike barua ya kuacha kazi.


“Sitaki utani kwenye mambo haya,msinijaribu,sipimiki,umealikwa kwenye kikao haujaja,kama mtendaji hayupo eneo la kazi basi aniambie kalazwa hospitali gani nije kumuona,ndiyo maana mmekuja hapa hata karatasi za vikao hamna,ni kikao chenu cha kwanza?,mmekuja kwenye kazi kweli au mmekuja kunijaribu?”,alihoji Telack.



Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alihamasisha wakazi wa mkoa huo kutumia mkaa unaotokana na mabaki ya mimea ikiwemo mapumba ya mpunga na matumizi ya gesi ili kuondokana na matumizi ya mkaa kwani inasababisha miti kukatwa ovyo.


Naye Afisa Malia asili wa mkoa wa Shinyanga Billie Edmot alisema wanaendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi kuanzisha vitalu vya miti ili kuondokana na hali ya janga sambamba na kama sehemu ya kujipatia ajira.


Katika kukabiliana na hali ya jangwa mkoani Shinyanga,wajumbe wa kikao hicho waliazimia kuwa kila kijiji,halmashauri na mkoa kuanzisha vitalu na misitu ya miti na kuhakikisha kuwa kila msimu wa mvua unapoanza wananchi wahamasishwa kupanda miti kwa wingi ikiwemo ya matunda. 
SIKILIZA HAPA CHINI SAUTI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MH. ZAINAB TELACK AKIWAFUNGUKIA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI BAADA YA KUMVURUGA

ANGALIA PICHA 18 WAKATI WA KIKAO CHA WADAU WA MAZINGIRA MKOA WA SHINYANGA KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA OFISI YA MKUU WA MKOA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akifungua kikao cha wadau wa Mazingira mkoani Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza katika kikao hicho

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiongoza kikao cha wadau,kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro

Kikao kinaendelea

Kikao kinaendelea

Wadau wa mazingira wakiwa ukumbini
Afisa Maliasili mkoa wa Shinyanga
Afisa Maliasili mkoa wa Shinyanga Billie Edmott akitoa taarifa kuhusu utunzaji mazingira mkoani Shinyanga

Kikao kinaendelea
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kahama
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kahama Mabala Mlolwa akichangia hoja
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akichangia hoja katika kikao hicho
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akichangia hoja katika kikao hicho


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje aliyemwakilisha mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akichangia hoja

Tunafuatilia kinachoendelea hapa

Kikao kinaendelea

Wadau wa mazingira wakiwa ukumbini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akichangia hoja ukumbini
Mshauri wa Mgambo mkoa wa Shinyanga
Mshauri wa Mgambo mkoa wa Shinyanga Luteni Kanali Prosper Massawe akichangia hoja

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifunga kikao cha wadau wa Mazingira,ambapo aliwataka watumishi wa serikali kujali muda katika utendaji kazi wao-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Nimekurekodia sauti ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akielekeza kukerwa na wakurugenzi wa halmashauri ambao hawakuhudhuria kikao chake...Bonyeza Play Hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527