MANENO YA UCHOCHEZI YANAYODAIWA KUMPONZA MBUNGE LEMA..LEO KAPANDISHWA KIZIMBANI


Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika kesi mbili tofauti.



Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”


Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano Septemba Mosi kinyume cha sheria.


Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.

Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.Kesi hiyo itatajwa tena Septemba

Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa ni Innocent Njau.


Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema magereza kwa madai kuwa wadhamini wamechelewa, lakini mbunge huyo alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527