Kijana Aliyeugua Ugonjwa Wa Kuzeeka Afariki Dunia



Kijana mmoja wa mjini Mumbai ambaye amekuwa akiugua ugonjwa usio kawaida wa jeni ambao huufanya mwili kuzeeka mara nane zaidi ya ilivyo kawaida amefariki dunia.

Nihal Bitla mwenye umri wa miaka 15 alikuwa mwanaharakati wa India anayefanya kampeni dhidi ya ugonjwa huo kwa jina Progeria.

Bitla aligonga vichwa vya habari alipokuwa akitafuta wagonjwa wengine 60 wanaougua ugonjwa huo ili kushiriki katika yake mjini Boston.Alianzisha mtandao wa kijamii kutoa hamasa kuhusu ugonjwa huo.

Hivi karibuni alianzisha hamasa kwa jina #HatsOnProgeria,ambapo alionekana na kundi moja la wafuasi wake katika kituo cha reli cha Chhatrapati Shivaji.

Bitla alipata umaarufu baada ya kukutana na nyota wa Bollywood Aamir Khan mnamo mwezi Disemba baada ya ukurasa wake wa facebook kuzungumzia kuhusu habari yake na swala kwamba alikuwa shabiki mkubwa wa nyota huyo.

Alifariki hospitalini siku ya Jumanne kusini mwa jimbo la Telangana,ambapo alikuwa ameenda kuhudhuria sherehe za harusi.

Ripoti za vyombo habari zinasema kuwa huenda alikosa maji mwilini kutokana na joto katika eneo hilo.
 
R.I.P Nihal

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527