Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada
ya basi la kampuni ya Kidia one lililokuwa likitokea jijini Dar es
Salaam kuelekea jijini Mwanza kugongana uso kwa uso na lori la mizigo
lililokuwa likitoka Dodoma kuelekea Morogoro katika kijiji cha vikonje
kata ya mtumba nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo
dereva msaidizi wa basi aliyejitambulisha kwa jina moja la Makubeli
akisema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi kuharibika mfumo wa breki
na kumshinda dereva mwenzake kauli inayopingana na mmoja kati ya abiria
aliyekuwemo kwenye basi hilo ambaye anadai chanzo ni mwendo kasi ambapo
dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita basi jingine lililokuwa mbele
yao bila tahadhari na ghafla akakutana uso kwa uso na lori.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Sasp David Misime amesema chanzo
cha ajali kimetokana na dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 663
AXL aina ya Scania alipokuwa akijaribu kulipita gari lingine bila
kuchukua tahadhari na kukutana uso kwa uso na lori lenye namba za
usajili T 496 CFG likiwa na tela namba T 576 AXZ ambapo watu wawili
waliofahamika kwa majina ya Fadhili Saidi dereva wa lori na Chogo
Chigunda utingo wa basi wakafariki dunia.
.png)

.png)
Social Plugin