
Wanachama wa MISA TAN wakiwa katika Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi) jijini Mwanza. Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa MISA Tanzania - Edwin Soko akizungumza Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) katika Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi).
Wanachama wa MISA TAN wakiwa katika Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi) jijini Mwanza.

Wanachama wa MISA TAN wakiwa katika mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Mwanza.
Wanachama wa MISA Tanzania wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya MV New Mwanza walipotembelea Bandari ya Mwanza, Oktoba 13, 2026.Wanachama wa MISA Tanzania wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya MV New Mwanza walipotembelea Bandari ya Mwanza, Oktoba 13, 2026.
Wanachama wa MISA TAN wakiwa katika mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Mwanza.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), wakiongozwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Edwin Soko, wametembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali jijini Mwanza, ikiwemo Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi) na mradi wa ujenzi wa meli kubwa ya kisasa ya MV New Mwanza katika Bandari ya Mwanza.
Ziara hiyo imefanyika Oktoba 13, 2026, siku moja baada ya kongamano la wadau wa habari kutoka taasisi za umma na sekta binafsi lililofanyika jijini Mwanza, Oktoba 12, 2026, kwa lengo la kujadili namna ya kutumia uandishi wa habari kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta mbalimbali na kuunga mkono juhudi za kuleta maendeleo nchini.
Kongamano hilo liliongozwa na kaulimbiu “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi” na kuwashirikisha wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kati, pamoja na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na sekta binafsi.
Kanda ya Ziwa inajumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera; Kanda ya Magharibi inajumuisha Kigoma, Tabora na Katavi, huku Kanda ya Kati ikijumuisha Singida na Dodoma.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa kuhusu mradi wa meli ya MV New Mwanza, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), Abdulrahman Ally, amesema meli hiyo ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi nchini kutokana na mchango unaotarajiwa katika kuboresha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo, pamoja na kuchochea shughuli za biashara katika Ukanda wa Ziwa Victoria.
Meli hiyo inatarajiwa kuimarisha mawasiliano na usafiri wa majini katika Ziwa Victoria, kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria na kuongeza fursa za mwingiliano wa kibiashara baina ya Tanzania na nchi nyingine zinazozunguka ziwa hilo.
Kwa upande mwingine, Daraja la John Pombe Magufuli, linalounganisha eneo la Kigongo na Busisi mkoani Mwanza, ni mradi muhimu wa miundombinu unaolenga kurahisisha usafiri na usafirishaji katika Ukanda wa Ziwa Victoria.
Daraja hilo linasaidia kupunguza utegemezi wa vivuko, kuokoa muda wa safari na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma. Hatua hiyo ina umuhimu katika kukuza biashara, kupanua fursa za uwekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia madhumuni ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema wameamua kutembelea miradi hiyo ya kimkakati ili kuwapa waandishi wa habari fursa ya kujionea maendeleo yake na kupata uelewa utakaowawezesha kuandika habari sahihi kuhusu uwekezaji na mchango wa miradi hiyo katika maendeleo ya nchi.
Amesema waandishi wa habari wana nafasi muhimu ya kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kuhabarisha umma kuhusu miradi inayotekelezwa nchini, fursa za kiuchumi zinazotokana nayo na namna inavyoweza kuchangia kuboresha maisha ya wananchi.
Ziara hiyo imewapa wanachama wa MISA Tanzania fursa ya kujionea miradi ya kimkakati inayohusisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, huku ikisisitiza umuhimu wa uandishi wa habari katika kuelimisha umma kuhusu uwekezaji, maendeleo ya kiuchumi na fursa zinazopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi.













































Social Plugin