Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AWASILI ARUSHA, KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo, Septemba 9, 2026, amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Huduma za Afya ya Msingi.

Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuanzia leo Septemba 09 hadi 11, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe   pamoja Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Mhe. Amos  Makala wameongoza viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Arusha.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com