Serikali imeweka mikakati ya kukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuongeza ufanisi, uwekezaji, ajira na mchango wake katika Pato la Taifa.
Mikakati hiyo inalenga kuchakata malighafi zinazozalishwa nchini na kuongeza thamani yake.
Hayo yamebainisha na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) wakati wa hafla ya 19 ya utoaji wa Tuzo kwa Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa Mwaka, Septemba 2, 2026 jijini Dar es Salaam.
Kapinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiwezesha sekta ya viwanda na kukuza maendeleo ya nchi. P
ia, ameishukuru CTI kwa kuandaa tuzo hizo.
Amesema tuzo hizo zimekuwa chachu kwa wazalishaji kushindana kwa tija, kuongeza ubora na kuboresha utendaji.
Ameongeza kuwa Wizara imekamilisha maandalizi ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda ya mwaka 2025 na Sera ya Maendeleo ya Jinsia ya mwaka 2023–2025.
Kwa mujibu wa Kapinga, Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 inahitaji msingi imara wa uzalishaji.
Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na kuimarisha uhusiano kati ya viwanda na sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini, misitu, nishati na huduma.
Amesema usindikaji wa rasilimali nchini utaongeza kipato cha wananchi, ajira na mapato ya Serikali. Hatua hiyo pia itapunguza uuzaji wa bidhaa ghafi nje ya nchi.
Kapinga ameahidi kushirikiana na CTI kuondoa vikwazo vinavyokwamisha uzalishaji. Pia, amewapongeza wazalishaji waliotunukiwa na kuwataka wengine kuendelea kujiboresha.















































Social Plugin