Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NG'OMBE AUA MTU HUKO NGOKOLO - SHINYANGA MJINI


Ng'ombe aliyesababisha kifo.
***
Mzee Monisa, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwinamila, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na ng’ombe katika tukio lililotokea Alhamisi, Septemba 3, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea baada ya watu kufika kumchukua ng’ombe huyo kwa ajili ya kwenda kumpandisha jike. Inadaiwa kuwa walipomfikia, ng’ombe huyo alikimbia hadi kwa jirani, eneo analoishi Mzee Monisa.

Mzee Monisa alichukua fimbo na kujaribu kumrudisha ng’ombe huyo, lakini ng’ombe huyo alimgeukia na kumkanyaga.

Baada ya tukio hilo, Mzee Monisa alikimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya matibabu ambapo imeelezwa kuwa Vipimo vilibaini kuwa alikuwa amevunjika mbavu na alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mzee Monisa pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo. 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi. Apumzike kwa amani.

Tutawaletea Taarifa KAMILI HIVI PUNDE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com