Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IFAD IMETEMBELEA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KUELENDELEZA KILIMO NA UVUVI (AFDP)



Na; Mwandishi Wetu-Geita


Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Pamoja na wataalam kutoka sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (Agriculture and Fisheries Development Programme – AFDP) hususan kutoka Sekta ya Uvuvi Wamefanya Mazungumzo na Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Bw. Munguanatosha Macha wakiwa katika sehemu ya ziara maalum ya Tathmini ya muda wa kati (MTR) ya kutembelea maeneo yanayotekeleza Programu hiyo.

Kikao hicho kimefanyika Septemba 2, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Baada ya kikao hicho timu hiyo ya wataalam ilipata nafasi ya kutembelea kituo cha uzalishaji na ukuzaji viumbemaji kilichopo Rubambagwe Wilayani Chato kwa ajili ya kutembelea miundombinu iliyowezeshwa na Programu ya AFDP kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa vifaranga pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji samaki wanaozunguka eneo hilo na maeneo ya karibu.


AFDP ni Programu inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu.

Na kutekelezwa na Wizara ya  Mifugo na Uvuvi, Shirika la Uvuvi nchini (TAFICO)Wizara ya Uchumi wa Buluu, Wizara ya Kilimo na baadhi ya Taasisi zake.

Programu hii inalenga kuimarisha uzalishaji na tija katika kilimo na uvuvi, kuongeza fursa za kipato na biashara, pamoja na kuimarisha minyororo ya thamani katika sekta hizo.

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com