Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC CHALAMILA NAOMBA NISAIDIE KUNA WATU WANATAKA KUNIDHULUMU ENEO LANGU-KIZENGA


Na Mwandishi Wetu

MKAZI wa mtaa wa Unyasini katika Kata ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam Yahaya Kizenga amemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Mkuu wa mkoa huo Albart Chalamila kuwasaidia kupata haki ya eneo la aridhi ambalo kuna watu wamevamia wakitaka kuwadhulumu.

Kwa mujibu Kizenga amesema amekuwa katika eneo hiki tangu mwaka 1976 ambalo alipewa na Nyerere wakati wa operesheni ya Nguvu Kazi na anayo hati ya Kijiji lakini cha kushangaza kuna watu wamejitokeza na kudai eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kizinga ambaye ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi amesema alipata eneo wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na amekuwa akiishi katika eneo hilo tangu mwaka huo wa 1976.

“Nimekuwa nikiishi hapa tangu mwaka 1976 na ninamiliki eneo hili nikiwa na hati ya Kijiji niliyopewa wakati huo. Mbali na kuwa na nyumba yangu lakini nimekuwa nimekuwa nikiliendeleza kwa shughuli za kilimo cha mbogamboga “

Akieleza zaidi kuhusu eneo hilo amesema cha ajabu alitokea mtu aliyekuwa anajulikana kwa jina la Juliana Lyimo ambaye alikuwa anamiliki kampuni ya Oliver beach Resorts akidai hili eneo ni lake.

“Baada ya kujitokeza kwa mtu yule mimi pamoja na majirani wenzangu wanne tuliamua kwenda Serikali ya Mtaa Kawe lakini hatukupata suluhu hivyo tukaenda Mahakamani na tunashukuru Mungu baada ya kuwasilisha vielelezo vyetu tulishinda kesi mwaka 2015.

“Baada ya kushinda kesi mahakamani tulikwenda kukazia hukumu lakini pia ilibidi na twende Wizara ya Aridhi kwasababu miaka ambayo nimekaa tangu tushinde kesi mwaka 2015 tulikaa mpaka 2021 na kila siku tukiuliza tunaambiwa kuna rufaa.

“Lakini nilishutuka kwanini kuna rufaa miaka yote,hivyo nikaamua kwenda Wizara ya Aridhi tena kuangalia na kukuta yule mmiliki ambaye tulimshinda mahakamani ndio amemilikishwa ,hiyo ilikuwa mwaka 2021.Na sasa tumeona watu wamekuja na kuanza kumwaga kifusi katika eneo hili lenye ukubwa wa heka moja na nusu.”

Kizenga amesema kutokana na umri wa utu uzima amekuwa akikabiliwa na maradhi yeye pamoja na mkewe na kutokana na uchumi duni umesababisha wajanja wachache wanataka kuwadhulumu eneo lao na kwamba wanaamini anayeweza kuwasaidia kupata haki yao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ambaye tumeshuhudia akitenda haki hasa kwa wake wasiokuwa na uwezo.

“Tunamuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pamoja na Mamlaka zinazohusika na utatuzi wa migogoro ya aridhi watusidie kupata haki yetu,hapa ni kwetu na tuko kihalali lakini leo hii wanakuja watu wanataka kutuondoa sasa wanataka twende wapi?

“Mkuu wa Mkoa tunakuomba utusaidie tupate haki yetu, sisi ni wazee tusio na kitu tunadhulumiwa.Ombi langu kwa mamlaka na viongozi wote watusikie kilio chetu.Wanaotaka eneo langu ni watu ambao wanafanya kila aina ya hila na mbinu na wapo tayari kufanya lolote kudhulumu”

Kwa upande wake Mariam Kizenga ambaye ni mke wa Mzee Kizenga amemuomba Rais DK.Samia Suluhu Hassan kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwasaidia ili eneo lao lisichukuliwe na watu ambao wameonekana wanafanya ujanja ili kuwadhulumu.

“Tunamuomba Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na viongozi wengine watusaidie kuna mtu amekuja hapa na kuanza kuweka kifusi cha mchanga,anataka kutudhulumu.Tuko hapa kwa miaka 50 tukidhulumiwa tunakwenda wapi? Na sisi hatuna uwezo wa kujenga na makazi yetu yako hapa kwa muda wote .Tunaomba Serikali itusaidie.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com