Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE AZZA AGUSA MAISHA YA WANANCHI NDUGUTI KWA VITENDO



Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akisalimia na wa wananchi wa Kijiji cha Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga
Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Wananchi wa Kijiji cha Nduguti Kata ya Nyida wilayani Shinyanga, wameelezea furaha yao kwa Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, kwa kuguswa na maisha ya wananchi wake na kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili kwa vitendo, ikiwamo kuwapaulia Zahanati ya kijiji hicho kwa fedha zake za mfukoni.

TAZAMA VIDEO👇👇


Wamebainisha hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Azza wa kusikiliza kero zao akiwa pia ameambatana na wataalamu wa serikali kujibu kero hizo.

Mmoja wa wanachi hao Ashura Manyama, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa kuwapaulia Zahanati ya kijiji hicho, ambalo boma lake limekaa kwa muda mrefu, na kusababisha kukosa huduma za matibabu karibu na maeneo yao.
“tunatoa shukrani kwa Mbunge wetu kwa kutupaulia Zahanati yetu ya kijiji cha Nduguti, tangu tumeanza kupata wabunge huyu diyo Mbunge wa kwanza kututendea haki,” amesema Ashura.

Aidha, wananchi hao wakiwasilisha kero mbalimbali kwa Mbunge huyo walilamikia pia suala ya ukosefu wa huduma ya majisafi na salama, umeme kwa baadhi ya vitongoji, pamoja na kuharibika kwa skimu ya umwagiliaji ya Nduguti.
Naye Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema amefika katika kijiji hicho, kutoa shukrani pamoja na kusikiliza kero zao, na kwamba baadhi ya kero ameshaanza kuzifanyia kazi, ikiwamo kutoa pesa yake mfikoni na kiupau Zahanati ya kijiji hicho.

Amesema, kwa hatua ilipofikia Zahanati hiyo, atakwenda kuisemea pia Serikalini, ili ikamilike na kuanza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi.

Akizungumzia pia kero ya umeme, amesema litafanyiwa kazi, na kwamba Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), inasema kuanzia 2025 hadi 2030, vitongoji vyote vya Nduguti vitakuwa na umeme.
“Katika vitongoji vya miezi sita, tulivyopata jimbo la Itwangi kuwekewa umeme, tumepata vitongoji 58 na kitongoji cha Nduguti tumepata Kitongoji kimoja, na vitongoji vilivyosalia navyo vitawekewa umeme, serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ipo kwa ajili ya wananchi wake,” amesema Azza.
Akizungumzia utatuzi wa Skimu ya Umwagiliaji, amesema licha ya kusubiri Serikali, bali atamtuma Katibu wake ili wafike kwenye eneo hilo, na kufanya tathimini ili wajenge kwa hatua za awali kwa ajili ya kuzuia maji yasipotee.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Itwangi Said Nasorro akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Itwangi Said Nasorro akizungumza kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akimfariji mjane ambaye anawatoto sita na alipata stroke ambapo alimsaidia kwa kumpatia pesa na kuahidi kuwa nunulia sare za shule na mahitaji yote watoto wake.
Zahanati ya kijiji cha Nguduti ambayo imepauliwa na Mbuge Azza kwa fedha zake za mfukoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com