Taka zinazozalishwa katika masoko zimeelezwa kuwa zinaweza kubadilishwa kuwa bidhaa zenye thamani na kuwa chanzo cha kipato.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa GEHESE, Liliani Lihundi, akizungumza wakati wa warsha ya uhamasishaji na kujenga uwezo kuhusu “Market Waste to Wealth” iliyofanyika Mbezi, Dar es Salaam, amesema usimamizi mzuri wa taka unaweza kusaidia kulinda mazingira na kuongeza fursa za kiuchumi.
Lihundi amesema taka za masokoni zinaweza kuchakatwa na kuzalisha mboji, chakula cha mifugo pamoja na bidhaa nyingine.
Amesema matumizi ya teknolojia mpya, ikiwemo Black Soldier Fly Larvae (BSFL), yanaweza kuongeza thamani ya taka za kikaboni.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbezi, Pius Ragiro Nyantori, amesema elimu ya utenganishaji taka inapaswa kupewa kipaumbele katika masoko na jamii.
Nyantori amesema Serikali itaweka mazingira yatakayowezesha kuanzishwa kwa vituo vya uchakataji taka katika masoko ya kata hiyo.
Amesema vituo hivyo vinaweza kuwa kichocheo cha ajira na biashara kwa vijana, wanawake na wafanyabiashara.
Mratibu wa Programu ya Taka ni Mali GEHESE, Catherine Sembua, ametoa mafunzo kuhusu usimamizi wa taka, aina mbalimbali za taka na umuhimu wa kuzitenganisha tangu zinapozalishwa.Sembua, ambaye pia ni mtafiti wa masuala ya usimamizi wa taka na mwanazuoni wa Shahada ya Uzamivu katika eneo hilo, amewataka wafanyabiashara wa masokoni kuanza kuziona taka kama fursa badala ya changamoto.
Amesema Kituo cha Ubunifu cha GEHESE kitaendelea kuwajengea uwezo wafanyabiashara na jamii kuhusu utenganishaji wa taka na namna ya kuzibadili kuwa rasilimali kupitia uchumi wa mzunguko (circular economy).
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Gender, Health and Sustainable Environment (GEHESE), Liliani Lihundi akizungumza wakati wa warsha ya uhamasishaji na kujenga uwezo kuhusu “Market Waste to Wealth” iliyofanyika Mbezi, Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya Mbezi, Pius Ragiro Nyantori, kizungumza wakati wa warsha ya uhamasishaji na kujenga uwezo kuhusu “Market Waste to Wealth” iliyofanyika Mbezi, Dar es Salaam
wanzilishi na Mwenyekiti wa Gender, Health and Sustainable Environment (GEHESE), Liliani Lihundi pamoja na Diwani wa Kata ya Mbezi, Pius Ragiro Nyantori, wakiteta jambo .





















Social Plugin