Na Sheila Ahmadi, Dodoma
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni inayojihusisha na uzalishaji wa mazao ya mboga mboga mkoani Iringa, Neema Mwamoto amesema uwezeshaji alioupata kupitia AGCOT umekuwa sehemu muhimu ya safari yake kutoka kuwa mkulima wa kawaida hadi kuanzisha kampuni inayolenga kukuza uzalishaji na masoko ya mazao ya kilimo.
Neema amesema kuwa safari yake katika kilimo ilianza akiwa mkulima wa kawaida, ambapo alianza kulima mazao mbalimbali kabla ya kuingia katika mfumo wa kilimo cha kibiashara na baadaye kufanya kazi kama mkulima mkataba katika kampuni ya (GBRI) mkoani Iringa mwaka 2015.
mwaka 2017 alianza kulima matikiti, huku mwaka 2019 akiendelea na shughuli za kilimo kupitia kampuni, hatua iliyomuwezesha kupata uzoefu zaidi kuhusu uzalishaji na masoko.
"uzoefu huo ulimsaidia kuona fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na kuanza kufikiria namna ya kuanzisha kampuni yake binafsi ili aweze kuzalisha kwa kujitegemea, badala ya kuendelea kufanya kazi kama mkulima mkataba.
Amesema mwaka 2021 changamoto zilizotokana na COVID-19 ziliathiri shughuli zake za kilimo, lakini baadaye alirejea na kuamua kuanzisha kampuni yake mkoani Iringa.
“Nilianza kama mkulima wa kawaida, lakini nilipoanza kufanya kazi kama mkulima mkataba nilianza kuona kuna fursa nyingi katika kilimo. Hapo ndipo nilipopata wazo la kuanzisha kampuni yangu binafsi ili niweze kulima na kukuza shughuli zangu,” amesema Mwamoto"
Katika Hatua nyingine Neema amesema kampuni hiyo ilipoanza, ilijikita zaidi katika kutafuta masoko ya ndani (local market), lakini ndoto yake ilikuwa kufikia hatua ya kuuza mazao katika masoko ya nje ya nchi (export market).
katika kufikia ndoto hiyo, amepitia michakato mbalimbali ya kujengewa uwezo kupitia wadau mbalimbali, ikiwemo AGCOT, ambao umekuwa sehemu ya safari yake ya kujifunza na kuboresha shughuli za kampuni.
uwezeshaji huo umemsaidia kupata uelewa zaidi kuhusu uzalishaji wa mazao kwa kuzingatia mahitaji ya soko, hatua ambayo imeendelea kumjengea uwezo wa kukuza biashara yake na kuwafikia wakulima wengine.
Aidha Dhumuni la sasa ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga, kuimarisha masoko na hatimaye kufikia soko la kimataifa.
Vilevile Neema ameongeza kuwa safari yake kutoka kuwa mkulima wa kawaida hadi kuwa mwanzilishi na mkurugenzi wa kampuni imeonyesha umuhimu wa uwezeshaji kwa vijana na wakulima, akisisitiza kuwa elimu, ujuzi, masoko na fursa za kibiashara ni muhimu katika kukuza sekta ya kilimo.
Nitaendelea kutumia uzoefu nilioupata pamoja na fursa za uwezeshaji kutoka kwa wadau kama AGCOT, kwa lengo la kukuza kampuni na kuchangia kuongeza kipato cha wakulima
.


Social Plugin