
Hivi karibuni, Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Accra ilimuhukumu Camilla Alhassan, mshawishi maarufu wa TikTok (Tiktoker), kifungo cha mwaka mmoja jerezani. Adhabu hii ilitolewa baada ya mshtakiwa kukiri makosa ya kusambaza taarifa za uongo na kufanya tabia ya kuudhi (offensive conduct) dhidi ya Rais John Dramani Mahama.
Kesi hii inaashiria hatua kubwa katika udhibiti wa maudhui ya kidijitali barani Afrika na inaibua maswali muhimu kuhusu mipaka ya uhuru wa kujieleza na wajibu wa kisheria wa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hukumu dhidi ya Alhassan inasimama juu ya misingi miwili mikuu ya kisheria inayolenga kulinda usalama wa jamii na sifa za watu
Mosi, Kusambaza Taarifa za Uongo (False News) - Sheria za Ghana zinakataza utengenezaji au usambazaji wa taarifa ambazo mtengenezaji anajua au ana sababu ya kuamini kuwa ni za uongo, hususan kama zinaweza kusababisha hofu au taharuki miongoni mwa jamii.
Pili, Tabia ya Kuudhi (Offensive Conduct) - Matumizi ya lugha au madai yanayolenga kudhalilisha, kuchochea chuki, au kuhatarisha amani ya umma—katika muktadha huu, kumhusisha kiongozi wa nchi na matendo ya ushirikina na kafara ya wanyama kwa malengo ya kisiasa.
Sakata hili linaangazia athari kubwa za mitandao ya kijamii katika nyanja za siasa na utulivu wa kijamii:-
Mmomonyoko wa Imani ya Kisiasa: Kudai kuwa Rais alifanya matambiko kwa kuzika ng'ombe 32 nchi nzima kulilenga kuchafua sifa yake na kupunguza uaminifu wake mbele ya wapiga kura, jambo linaloweza kuathiri mchakato wa kidemokrasia.
Silaha ya Algorithm na Ushawishi: Kama "Tiktoker," Alhassan alitumia nguvu ya ushawishi wake (clout) kupata watazamaji wengi. Katika zama za kidijitali, taarifa za kusisimua na za uzushi husambaa haraka kuliko ukweli, jambo linalofanya madhara yake kuwa makubwa na ya haraka.
MAANA YA HUKUMU HII KWA MUSTAKABALI WA KIDIJITALI (IMPLICATIONS)
Uamuzi wa Jaji kukataa ombi la mawakili wa Alhassan la kupunguza adhabu una ujumbe mzito
Mahakama imeweka wazi kuwa umaarufu wa mtandaoni (social media fame) sio ngao dhidi ya sheria. Kifungo hiki kinatumika kama onyo kwa waundaji wengine wa maudhui (content creators) kuwa uhuru wa kujieleza unaambatana na wajibu.
Aidha, Kesi hii inaongeza msukumo kwa serikali za Kiafrika kuimarisha mifumo ya kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya uhalifu wa kimtandao (cybercrime).
USHAURI WANGU
Hukumu ya Camilla Alhassan ni kielelezo cha namna mifumo ya sheria inavyolazimika kubadilika ili kukabiliana na changamoto mpya zinazoletwa na teknolojia.
Wakati mitandao ya kijamii ikiendelea kuwa jukwaa kuu la mijadala ya umma, kesi hii inakumbusha jamii kuwa maneno yana madhara ya kisheria, na kwamba ulimwengu wa kidijitali unapaswa kuongozwa na ukweli, maadili, na heshima kwa utu wa wengine.
Kama Tanzania Tuna paswa kuchukua hatua za wazi kwa wahalifu wa mitandao na kama nilivyo shauri mara zote tunaweza kupitia hatua tatu ili tuweze kukuza uelewa kwa wananchi na hatimae watakao kaidi zaidi tuwawajibishe kwa mujibu wa sheria za nchi
Hatua ya Kwanza : Wahalifu wakwamatwe na kwa uwazi watangazwe na kuonywa kisha waachiwe - Hii itakua somo kwa wengine ambao wana kawaida ya kufata mkumbo kwenye kutenda uhalifu wa kimtandao na wakidhani serikali imelala
Hatua Ya Pili: Mhalifu anapo rudia akamatwe tena kwa uwazi na kulipishwa faini kwa mujibu wa sheria zetu - Pesa zitakazo patikana kwneye hili ziwekwe kwenye mfuko maalum utakao saidia kuimarisha udhibiti wa uhalifu mtandao kupitia elimu ya uelewa na nyezo nyingine za udhibiti
Hatua ya tatu: Mhalifu anapo rudia mara ya tatu kunakua hakuna tena namna ila ni kufungwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu na hili liwe somo kwa wengine wote.
Naomba kuwasilisha.
Yusuph Kileo ,
Mtaalam wa usalama mtandao na Uchunguzi wa makosa ya Kidigitali
Dar Es Salaam, Tnazania
19 - July - 2026.
Social Plugin