Makubwa Haya: DIWANI APENDEKEZA WAFANYAKAZI WA MANISPAA WAPEWE SAA MOJA YA KUFANYA NGONO KILA WIKI

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyakazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki
****

Madiwani katika baraza la mji mdogo wa Sweden wamepinga muswada wa pendekezo la kuwapa wafanyikazi wa manispaa wanaolipwa, 'mapumziko ya kufanya tendo la ngono'

Per-Erik Muskos, diwani wa Övertorneå alipendekeza kuwapatia wafanyakazi hao mapumziko ya saa moja kila wiki kwenda nyumbani na kupata wakati bora wa kujamiana na wapenzi wao.

Aliambia BBC lengo kuu lilikuwa kuimarisha uhusiano baina ya watu.

''Ni jina la herufi tatu{Sex} , ''Bw Muskos aliposema mwezi Februari , akipuuzilia mbali pendekezo la kwamba anaingililia maisha ya watu binafsi.

Lakini wanachama wa baraza hilo ambao ni wahafidhina walipinga wazo hilo.

Meya wa Övertorneå, Tomas Vedestig, alihitimisha kwa kusema maisha ya kibinafsi ya wafanyikazi yanastahili kuwachwa vile yalivyo.

''Si kazi ya baraza kuingililia,'' aliambia SVT.

Bw Muskos alitumai kwamba kichwa cha mpango wa unyakuaji ungeongeza idadi ya watu katika mji wake ambao kwa hivi sasa idadi hiyo imezidi kushuka.

Mji wa Övertorneå kwa hivi sasa ni eneo ambalo lina watu 4,500 lakini wengi wao ni mwenye umri wa wastani.

''Vijana wengi huondoka mji huo pindi tu wanapo kamilisha masomo yao ,''Kasela amesema.

Pia anadhani kwamba kutenga saa moja kwa wiki kutawasaidia wanandoa ambao hawana wakati na wapenzi wao.

''Watu wana vitu vyengine vingi vya kufanya ,'' alisema. Ukiwa nyumbani watu wako kwenye mitandao, unahitajika kuwapeleka watoto kushiriki katika michezo ya soka na mpira wa magongo ya barafu , watu hawana wakati wa kulinda kila mmoja na kuwa na wakati bora bila watoto.

Iwapo wafanyikazi wa 550 wa baraza wamekasirika, itakuwa afueni kupata njia ya kutoa hasira katika hali hiyo mbaya: kwa sasa wana saa moja kwa wiki kushiriki katika michezo tofauti.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527