Video: MBUNGE WA NKASI ACHEKELEA ROMA KUPEWA KIBANO...ATAKA WASANII WANAOMTUKANA RAIS WAPEWE KIBANO ZAIDI


Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo

Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa.

"Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho halafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa?, aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachia mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy

Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikia  huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.

"Ukiusikia huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana, haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule halafu unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine, nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy

TAZAMA VIDEO HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527