KITILA MKUMBO : UKIPEWA KAZI NA MKUU WA NCHI,UNAIPOKEA NA UNAIFANYA KWA BIDII.....

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kitila Mkumbo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo akichukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu.

Prof. Mkumbo ambaye pia ni kada na mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Rais amempa heshima kubwa kwa nafasi hiyo, na yeye kama mtumishi wa umma hawezi kuikataa kwa kuwa ni kazi aliyotumwa na mkuu wa nchi.

"Ukishapewa kazi na mkuu wa nchi, unaipokea na unaifanya kwa bidii kama yalivyo matarajio, kwahiyo nimepokea uteuzi, nimekubali, mkuu wa nchi akikupa kazi utaikataa vipi, mkuu wa nchi akikupa kazi unaifanya, kumbuka mimi ni mtumishi wa umma" Amesema Prof Kitila

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527