MHUBIRI ALIYEKUWA AMEOA WANAWAKE 86 AMEFARIKI DUNIA..AMEACHA WATOTO 203


Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye aliyekuwa na takribani wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.

Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa

Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.

Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.

Wengine wao walikuwa wajawazito.

BBC iliripoti mwaka 2008 kuwa alikuwa na takriban watoto 170 lakini gazeti hilo lilisema kuwa aliwaacha watoto 203.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527