Maajabu! MTOTO AOTA MIZIZI KAMA MTI USONI


Mtoto Sahana Khatum kutoka nchini Dakar ameota mizizi usoni.

Wakati vitu visivyokuwa vya kawaida vilipomea kwenye uso wa Sahana Khatum, mwenye umri wa miaka 10 miezi minne iliyopita, babake hakushikwa na wasi wasi.

Lakini wakati vitu hivyo vilianza kusambaa, alishikwa na wasi wasi na kumlazimu kutoka kijijini mwake na kuelekea mji mkuu wa Bangladesh Dakar, kutafuta matibabu.

Madaktari sasa wanahofu kuwa Sahana huenda akawa mtoto wa kike wa kwanza kukumbwa na tatizo linalojulikana kama "tree man syndrome".

Ikiwa uchunguzi utabainisha hivyo, atakuwa mmoja wa watu wachache duniani walio katika hali hiyo.

Ni hali ya kijenetiki isiyokuwa ya kawaida ambapo mti humea hususan kwenye mikono na miguu.

Ni watu wachache ambao wote ni wanaume wanaoaminiwa kuwa na ugonjwa huo.

Mikono yote ya Abul Bajandar ilimezwa na miti iliyomea yenye uzito hadi kufikia kilo tano

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa raia wa kwanza wa Bangaladesh kupatikana na ugonjwa huo, kwa saa amefanyiwa upasuaji mara 16 na anaweza kuitumia mikono yake.

Madaktari wale wale waliomfanyia upasuaji Abul Bajandar, tena wanaendesha uchunguzi kubaini ikiwa Sahana anaugua ugonjwa sawa na huo.

Babake Sahana Mohammad Shahjahan ana matumaini kuwa madaktari watamtibu mtoto wao.

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527