JAMAA AMUUA KWA RISASI MFANYAKAZI WA SHAMBA AKIDHANI NI MNYAMA "NGIRI"


Watu nchini Afrika Kusini wamegadhabishwa, kufuatia taarifa za mwanamme mmoja, ambaye analaumiwa kwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyakazi wa shamba, akidhani kuwa mtu huyo ni ngiri.

Stephen Hepburn alifikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka ya mauaji.

Yeye na mwenzake wa kike walikuwa wakiwawinda ngiri kwenye shamba moja lililo mkoa wa Limpopo kaskazini siku ya Jumamosi, wakati Jan Railo ambaye alikuwa na umri wa miaka 23 aliuawa.

Msemaji wa Polisi Motlafela Mojapelo aliiambia BBC kuwa Bwana Hepbaun, alikamatwa siku ya Jumatutu.

Mojapelo aliongeza kusema kuwa bwana Hepburn alisema kuwa aliafyatua risasi eneo ambapo alisikia sauti alipokuwa akiwinda, na alipoenda kuangalia akapata kuwa ni mtu alikuwa amelala chini.

Wanachama wa tawi la chama cha ANC eneo hilo ambao waliofika mahakamani walisema hawaamini ikiwa mauaji hayo yalikuwa ya kimakosa.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527